Chapisha

Kurekebisha mfumo wa sauti

Baada ya kuunganisha mfumo wa sauti kwenye TV, rekebisha sauti towe ya TV kutoka kwenye mfumo wa sauti.

Kurekebisha mfumo wa sauti uliounganishwa na kebo ya HDMI au kebo optiki ya dijitali

  1. Baada ya kuunganisha TV kwenye mfumo wako wa sauti, bonyeza kitufe cha ACTION MENU, kisha uchague [Vipaza sauti] — [Mfumo wa sikizi].
  2. Washa mfumo wa sauti uliounganishwa, kisha rekebisha sauti.
    Ukiunganisha kifaa kinachoingiana na BRAVIA Sync ukitumia muunganisho wa HDMI, unaweza kukiendesha kwa kutumia rimoti ya TV tu.

Kumbuka

  • Unahitaji kusanidi mipangilio ya [Zao la sauti dijito] kulingana na mfumo wako wa sauti. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Zao la sauti] — [Zao la sauti dijito].
  • Kama mfumo wa sauti hautangamani na Dolby Digital au DTS, weka [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Zao la sauti] — [Zao la sauti dijito] kwenye [PCM].

Kidokezo

Kurekebisha mfumo wa sauti uliounganishwa na kebo ya sauti

  1. Baada ya kuunganisha TV kwenye mfumo wako wa sauti, bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Zao la sauti] — [Zao la Spika za Kivalia Kichwani/Sikizi] — [Zao la sauti (Halibadiliki)].
  2. Washa mfumo wa sauti uliounganishwa, kisha rekebisha sauti.

Kumbuka

  • Kama mfumo wa sauti hautangamani na Dolby Digital au DTS, weka [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Zao la sauti] — [Zao la sauti dijito] kwenye [PCM].

Kidokezo

  • Wakati unatumia mfumo wa sauti wa nje, sauti towe ya TV inaweza kudhibitiwa kwa kutumia rimoti ya TV ikiwa [Zao la Spika za Kivalia Kichwani/Sikizi] imewekwa kwa [Zao la sauti (Hubadilika)]. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Zao la sauti] — [Zao la Spika za Kivalia Kichwani/Sikizi] — [Zao la sauti (Hubadilika)].
  • Wakati unaunganisha subwoofer, bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Zao la sauti] — [Zao la Spika za Kivalia Kichwani/Sikizi] — [Subwoofer].