Chapisha

Kuunganisha vifaa vya Bluetooth

Kulinganisha TV na kifaa cha Bluetooth

Ni za modeli zinazokubali Bluetooth A2DP pekee ndizo ambazo zinaweza kutumia vifaa vya sauti vya Bluetooth.

Modeli zinazokubali Bluetooth A2DP ambazo hutumia vifaa vya sauti vya Bluetooth ndizo zina [Mlandanisho wa A/V] katika [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Zao la sauti].

  1. Washa kifaa cha Bluetooth na ukiweke katika modi ya kuoanisha.
    Ili kuweka kifaa chako cha Bluetooth katika modi ya kuoanisha, rejelea mwongozo wa maagizo wa kifaa.
  2. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Kiungambali na Vifaa vya Ziada] — [Mipangilio ya Bluetooth] — [Ongeza kifaa] ili uweke TV katika hali ya kuoanisha.
    Orodha ya vifaa vinavyopatikana vya Bluetooth itaonekana.
  3. Chagua kifaa unachokitaka kutoka kwenye orodha, kisha ufuate maagizo kwenye skrini.
    Ukiombwa kuweka msimbosiri, rejelea mwongozo wa maagizo wa kifaa.
    Baada ya uoanishaji kukamilika, kifaa kinaunganisha kwa TV.

Ili kuunganisha kifaa kilicholinganishwa cha Bluetooth

  1. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Kiungambali na Vifaa vya Ziada] — [Mipangilio ya Bluetooth].
  2. Chagua kifaa kilicholinganisha lakini hakijatenganishwa kutoka kwenye orodha.
  3. Teua [Unganisha].