Chapisha

Ikiwa uwekaji upya kamili (kuanzisha upya) wa TV unahitajika

Ikiwa una tatizo kama picha kutoonyesha kwenye skrini au rimoti kutofanya kazi, weka upya TV kwa kutumia utaratibu unaofuata. Ikiwa tatizo litaendelea, jaribu utaratibu wa kurejesha mipangilio ambayo TV ilitoka nayo kiwandani hapa chini.
Ikiwa kifaa cha nje cha USB kimeunganishwa kwenye TV, tenganisha kifaa cha USB kwenye TV kabla ya kuweka upya.

Weka upya kwa Kuzima

  1. Washa TV upya kwa kutumia rimoti.
    Bonyeza na ushikilie kitufe cha nishati kwenye rimoti kwa karibu sekunde 5 hadi ujumbe wa “Imezimwa” uonyeshwe.
    TV itazimika kisha kuwaka kiotomatiki baada ya karibu dakika moja.
  2. Chomoa kebo ya umeme ya AC (kebo kuu).
    Tatizo likiendelea baada ya hatua ya 1, chomoa waya wa kuwasha TV (kebo kuu) kwenye towe ya umeme. Kisha ubonyeze kitufe cha nishati kwenye TV na usubiri kwa dakika 2 na uchomeke waya wa nishati (kebo kuu) kwenye towe ya umeme.

Kidokezo

Mipangilio yako ya kibinafsi na data haitapotea baada ya TV kuwasha upya.

Kurejesha mipangilio ya kiwandani

Ikiwa tatizo litaendelea baada ya kuweka upya kwa kuzima, jaribu kurejesha mipangilio iliyotoka nayo kiwandani.

Kumbuka

Kuweka upya mipangilio ya kiwandani kuutaondoa data na mipangilio yote ya televisheni (kama vile Wi-Fi na maelezo ya kuweka mipangilio ya mtandao, Google akaunti na maelezo mengine ya kuingia katika akaunti, Google Play na programu zingine zilizowekwa).

  1. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Mapendeleo ya Kifaa] — [Weka upya] — [Kurejesha mipangilio ya kiwandani].
  2. Teua [Futa kila kitu].
    Ikiwa umeweka nambari ya PIN kwenye TV yako, utaulizwa uingize unapochagua [Futa kila kitu].
    Baada ya mchakato wa kurejesha mipangilio iliyotoka nayo kiwandani kufanikiwa, TV itaendelea na utaratibu Usanidi wa Kwanza. Unapaswa kukubali Google Masharti ya Huduma na Google Sera ya Faragha.