Chapisha

Huwezi kuunganisha kwa Intaneti, lakini sio kwa programu na huduma nyingine.

  • Mipangilio ya tarehe na saa ya TV hii huenda isiwe sahihi. Kulingana na programu na huduma nyingine, huenda usiweze kuunganisha kwenye programu na huduma hizo ikiwa saa si sahihi.
    Ikiwa saa si sahihi, bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — wezesha [Tumia saa ya mtandao] katika [Mapendeleo ya Kifaa] — [Tarehe na saa] — [Saa na tarehe otomatiki].
  • Hakikisha kwamba kebo ya LAN na waya ya nishati ya AC (waya kuu) ya kipanga njia/modemu* imeunganishwa vizuri.
    * Kipanga njia/modemu yako lazima iwekwe ili iunganishe kwenye Intaneti. Wasiliana na mtoa huduma wako wa Intaneti kwa mipangilio ya kipanga njia/modemu.
  • Jaribu kutumia programu baadaye. Seva ya mtoa maudhui ya programu huenda isiwe inafanya kazi.

Kidokezo

  • Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya usaidizi ya Sony.
    Tovuti ya Msaada