Chapisha

TV haiwezi kuunganisha kwenye Intaneti/Mtandao.

Ikiwa mtandao wa pasiwaya hauunganishi au unakatika, jaribu ifuatayo.

  • Bonyeza kitufe cha HOME na ukague kwamba mpangilio ufuatao umewezeshwa.
    [Mipangilio] — [Mtandao na Intaneti] — [Wi-Fi]
  • Angalia mahali pa usakinishaji wa TV na kipanga njia pasiwaya. Hali ya ishara inaweza kuathiriwa na hali zifuatazo:
    • Vifa vingine pasiwaya, kipasha jito, mwangaza wa floresenti, n.k., vinawekwa karibu.
    • Kuna sakafu au kuta kati ya kipanga njia pasiwaya na TV.
  • Zima na uwashe tena kipanga njia pasiwaya.
  • Ikiwa jina la mtandao (SSID) la kipanga njia pasiwaya ambacho unataka kuunganisha hakijaonyeshwa, chagua [(Kuingizaji kwa Mkono)] ili uingize jina la mtandao (SSID).

Ikiwa tatizo halitatatuliwa hata baada ya taratibu hapa juu au ikiwa huwezi kuunganisha hata na mtandao wa waya, angalia hali ya muunganisho wa mtandao.

Kuangalia hali ya muunganisho wa mtandao

  1. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Mtandao na Intaneti] — [Hali ya Mtandao] — [Angalia Unganisho].
    Angalia miunganisho yako ya mtandao na/au mwongozo wa seva upate maelezo ya muunganisho, au wasiliana na mtu ambaye anasanidi mtandao (msimamizi wa mtandao).

Kidokezo

  • Suluhisho utofautiana kulingana na ukaguzi wa hali ya mtandao. Kwa suluhisho za kila tatizo, angalia “Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara”kwenye Tovuti ya Usaidizi ya Sony.

Kumbuka

  • Ikiwa kebo ya LAN imeunganishwa kwenye seva amilifu na TV imepata nwani ya IP, angalia miunganisho ya seva yako na usanidi.

    Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Mtandao na Intaneti] — [Hali ya Mtandao].