Chapisha

Hauwezi kutumia kifaa cha USB HDD. (modeli za kurekodi kwa USB HDD pekee)

Modeli za kurekodi USB HDD zina [Usanidi wa kifaa cha kurekodi] katika [Mipangilio] — [Kutazama runinga].

  • Kagua kwamba kifaa cha USB HDD:
    • kimeunganishwa vizuri.

      Hakikisha kuwa imeunganishwa kwenye kituo cha USB3 cha bluu kilichotia lebo kuwa “HDD REC”.

    • kimewashwa.
    • kimesajiliwa kwenye TV.

      Ili kusajili kifaa cha USB HDD kwenye TV, bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Kutazama runinga] — [Usanidi wa kifaa cha kurekodi] — [Usajili wa HDD].

  • Kuunganisha kifaa cha USB HDD kupitia kituo cha USB hakukubaliwi.
  • Tekeleza [Ukaguzi wa utendaji wa HDD] ili ukague kwamba ainisho za USB HDD zinafikia mahitajiko.
    Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Kutazama runinga] — [Usanidi wa kifaa cha kurekodi] — [Ukaguzi wa utendaji wa HDD].