Kifaa cha USB HDD hakiwezi kusajiliwa. (modeli za kurekodi kwa USB HDD pekee)
Teua kwenye maandishi ili uruke hadi kwenye skrini husika ya mpangilio.
- Kagua kama kifaa cha USB HDD kimeunganishwa kwenye kituo cha USB3 (bluu) kilichoashiriwa kama “HDD REC”.
- Kama kifaa cha USB HDD kimeunganishwa vizuri kwenye kituo cha USB3 cha bluu, kisajili kwa ajili ya kurekodi tena kwa sababu kimesajiliwa tayari kama kifaa kwa malengo mengine kando na kurekodi (kama vile hifadhi).
Kumbuka
- Ikiwa kuna vifaa vilivyounganishwa kwenye vituo vya USB1 na USB2, viondoe kwa muda mfupi wakati unasajili USB HDD.