Chapisha

Vipengele vya ufikiaji

TV hii ina vipengele vya ufikiaji katika [Ufikiaji] kama vile ubadilishaji wa matini kuwa usemi kwa matini yaliyo kwenye skrini, kukuza ili kufanya matini kuwa rahisi kusoma, na manukuu.

Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Mapendeleo ya Kifaa] — [Ufikiaji] ili usanidi vipengele vya kumsaidia mtumiaji.

[Ufikiaji] ina kitendaji cha njia ya mkato ili uweze kukiwasha au kukizima kwa kubonyeza na kushikilia kitufe cha (Nyamazisha) kwenye rimoti kwa sekunde 3.

Kidokezo

  • Ili kubadilisha kipengele cha njia ya mkato, wezesha [Njia mkato ya ufikiaji] katika [Ufikiaji] na ubadilishe kutumia [Huduma ya njia ya mkato].
  • Ili utumie ubadilishaji wa matini kuwa usemi kwenye Mwongozo wa Usaidizi, tazama Mwongozo wa Usaidizi katika tovuti ya usaidizi ya Sony kwa kutumia kompyuta au simu maizi.

    http://www.sony-asia.com/support/
    QR code for the Sony support website
    http://www.sony-asia.com/support/