Chapisha

Kutazama picha katika mwonekano wa 4K (modeli za 4k pekee)

Unaweza kuunganisha kamera ya picha/kamkoda ya dijitali ambayo inakubali 4K towe ya HDMI hadi HDMI IN ya TV ili kuonyesha picha zenye mwonekano wa juu zilizohifadhiwa kwenye kamera. Unaweza pia kuonyesha picha zenye mwonekano wa juu zilizohifadhiwa katika vifaa vilivyounganishwa vya USB au mtandao wako wa nyumbani. Picha yenye mwonekano wa 4K au wa juu zaidi inaweza kuonekana katika mwonekano wa 4K (3840x2160).

Upatikanaji wa kitendaji hiki unategemea modeli/eneo/nchi yako.

Illustration of images from various devices displayed on the TV
  1. Kamera ya dijitali ya picha
  2. Kamkoda
  3. Kifaa cha USB
  4. Kifaa cha mtandao

Ili uangalie picha zilizohifadhiwa kwenye kifaaa cha USB au kifaa cha mtandao katika mwonekano wa 4K

  1. Unganisha kifaa cha USB au kifaa cha mtandao kwenye TV.
  2. Bonyeza kitufe cha HOME, chagua (aikoni ya Programu) kutoka kwenye Menyu ya mwanzo, kisha uchague [Kicheza Media].
    Ikiwa rimoti iliyokuja nayo ina kitufe cha APPS, unaweza kubonyeza kitufe cha APPS.
  3. Chagua jina la kifaa cha USB au jina la kifaa cha mtandao.
  4. Chagua folda, na kisha uchague faili ya kucheza.

Kutazama picha zilizohifadhiwa kwenye kamera ya picha/kamkoda ya dijitali

  1. Unganisha kamera tuli ya dijitali au kamkoda ambayo inakubali HDMI towe kwa jeki (soketi) ya HDMI IN ya TV kwa kutumia kebo ya HDMI.
  2. Bonyeza kitufe cha (Weka uteuzi) kwa kurudia ili kuteua kifaa kilichounganishwa.
  3. Weka kifaa kilichounganishwa kwa 4K towe.
  4. Anzisha uchezaji kwenye kifaa kilichounganishwa.

Kukagua fomati za faili zinazokubaliwa

Kutazama picha katika mwonekano wa 4K wenye ubora wa juu

Unaweza kuweka Umbizo la wimbi la HDMI kwa Umbizo lililoboreshwa ili utazame picha katika mwonekano wa 4K wenye ubora wa juu.

Kwa maelezo kuhusu Umbizo lililoboreshwa au kubadilisha mipangilio, rejelea ukurasa wa Mipangilio ya kutazama picha katika mwonekano wa 4K wenye ubora wa juu (modeli za 4k pekee).

Kumbuka

  • Picha ya 3D haiwezi kuchezwa.
  • Ukibadilisha picha kwa kubonyeza vitufe vya (Kushoto) / (Kulia), huenda ikachukua muda kuonyesha.