Kitufe cha EXT.BOX MENU kwenye rimoti hakifanyi kazi.
Teua kwenye maandishi ili uruke hadi kwenye skrini husika ya mpangilio.
Kipengele hiki kinapatikana kwa TV ambazo rimoti iliyojumuishwa ina kitufe cha EXT.BOX MENU.
Modeli zinazotangamana na IR Blaster zina [Usanidi wa IR Blaster] katika [Mipangilio] — [Kutazama runinga] — [Ingizo za nje].
- Ili utumie kitufe cha EXT.BOX MENU, unganisha na usanidi IR Blaster (kwa modeli zilizotolewa na IR Blaster). Unganisha IR Blaster, bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Kutazama runinga] — [Ingizo za nje] — [Usanidi wa IR Blaster]. (Huenda modeli zinazotangamana za IR Blaster zisipatikane kulingana na modeli/nchi yako.)
- Kama kifaa kinachotangamana na BRAVIA Sync-kimeunganishwa na kuonyeshwa kwa kutumia ingizo la HDMI, baadhi ya modeli zinaweza kuonyesha menyu kwa kutumia kitufe cha EXT.BOX MENU, lakini matumizi hayahakikishwi kwa vifa vyote.