Chapisha

Kusogeza programu kwenye kifaa cha kumbukumbu cha USB

Unaweza kusogeza programu zilizopakuliwa kwenye kifaa cha kumbukumbu cha USB ili uongeze nafasi inayopatikana kwenye TV.

Kumbuka

  • Unapoumbiza kifaa cha kumbukumbu cha USB, data yote iliyohifadhiwa kwenye kifaa cha kumbukumbu cha USB itafutwa. Cheleza data yako muhimu kabla ya kuumbiza.
  • Kutekeleza utaratibu huu huumbiza kifaa cha kumbukumbu cha USB ili kiweze kutumiwa na TV pekee. Kwa hivyo, huenda usiweze kutumia kifaa cha kumbukumbu cha USB na kompyuta, n.k.
  • Baaadhi ya programu haziwezi kuhamishwa kwenye kifaa cha kumbukumbu cha USB.
  1. Unganisha kifaa cha kumbukumbu cha USB kwenye TV.
  2. Bonyeza kitufe cha HOME, teua [Mipangilio] — [Kuhifadhi na kuweka upya] — kifaa unachokitaka cha kumbukumbu ya USB.
  3. Kiumbize kama kifaa cha ndani cha hifadhi.
  4. Uumbizaji unapokamilika, bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Programu].
  5. Chagua programu ambayo unataka kusogeza kwenye kifaa cha kumbukumbu cha USB.
  6. Chagua kifaa cha kumbukumbu cha USB kwenye hifadhi iliyotumiwa. Programu uhamishwa kwenye kifaa cha kumbukumbu cha USB.

Kidokezo

  • Rudia hatua ya 4 hadi ya 6 ili usogeze programu za ziada kwenye kifaa cha kumbukumbu cha USB.

Ili uondoe kifaa cha kumbukumbu cha USB

  1. Bonyeza kitufe cha HOME teua [Mipangilio] — [Kuhifadhi na kuweka upya] — kifaa unachokitaka cha kumbukumbu ya USB, na kisha uteue chaguo la kuliondoa.

Kumbuka

  • Kifaa cha kumbukumbu cha USB hutumiwa tu kuhifadhi programu. Ili utumie kifaa cha kumbukumbu cha USB kwa malengo mengine, lazima ukiumbize tena.
  • Ukifuata programu katika kifaa cha kumbukumbu cha USB kwa kutumia kompyuta, hutaweza kuianzisha kwenye TV.
  • Ukiondoa kifaa cha kumbukumbu cha USB kwenye TV, hutaweza kutumia programu ambayo ilihamishwa kwenye kifaa cha kumbukumbu cha USB.
  • Huwezi kubainisha kifaa cha kumbukumbu cha USB kama eneo la usakinishaji la programu. Kwanza sakinisha programu kwenye TV kama kawaida, na kisha uisogeze kwenye kifaa cha kumbukumbu cha USB.