Chapisha

Kuonyesha picha katika skrini ndogo

Unaweza kuonyesha picha ambazo unatazama (vipindi vya TV au maudhui kutoka vifaa vilivyounganishwa vya HDMI) kama skrini ndogo kwenye kona.

Mkao wa skrini ndogo hutofautiana kulingana na TV yako.

Illustration of a small screen displayed on the TV screen

Kumbuka

  • Huwezi kutumia [Picha ndani ya picha] kwenye TV na herufi ā€œCā€ mwishoni mwa jina la modeli.

Kuonyesha picha kama skrini ndogo

  1. Bonyeza kitufe cha ACTION MENU unapokuwa ukitazama vipindi vya TV au maudhui kwenye kifaa cha HDMI, na kisha uteue [Picha ndani ya picha].
    Picha ya sasa huonyeshwa kama skrini ndogo kwenye kona.

Kumbuka

  • Skrini ndogo huonyeshwa juu ya programu iliyotumika mwisho. Hata hivyo, programu inayoonyeshwa inaweza kutofautiana kulingana na hali nyingine.
  • Matumizi kama vile kubadilisha kituo hulemazwa unapokuwa ukitazama kwa kutumia skrini ndogo.
  • Vipindi vya TV, ingizo la nje kama vile kifaa cha HDMI, programu ambazo hucheza filamu, au baadhi ya programu ambazo zinaweza kucheza picha au muziki haziwezi kuonyeshwa kwa wakati mmoja.
  • Mkao wa skrini ndogo hurekebishwa kiotomati. Huwezi kuuweka wewe mwenyewe.

Kufunga skrini ndogo au kurejea kwenye skrini nzima

  1. Bonyeza kitufe cha HOME ili uonyeshe Menyu ya Mwanzo.
    Ujumbe wa skrini ndogo huonyeshwa juu ya skrini.
    Illustration of a list of recently used apps and a small screen displayed on the TV screen
  2. Katika ujumbe kwenye skrini ndogo, chagua [Fungua].
  3. Tumia vitufe chini ya skrini ndogo ili ufunge skrini ndogo au urejee kwenye skrini nzima.
    Picha iliyo hapa chini ni mfano wa kuona na inaweza kutofautiana na skrini halisi.
    Illustration of a list of recently used apps and a small screen displayed on the TV screen