Chapisha

Kuchagua ingizo

Ili utumie vifaa (kama vile vichezaji vya Blu-ray/DVD) vilivyounganishwa kwenye TV, au kutazama TV baada ya matumizi kama hayo, utahitajika kubadilisha ingizo.

  1. Bonyeza kitufe cha (Weka uteuzi) mara kwa mara ili uteue kifaa kilichounganishwa.

Kidokezo

  • Ili kubadilisha mpangilio au kuficha kipengee kilichoonyeshwa, bonyeza na ushikilie kitufe cha (Weka) kwenye rimoti na kipengee hicho kikiwa kimeangaziwa, na [Sogeza] na [Ficha] itaonyeshwa. Ukichagua [Sogeza], tumia (Kushoto) / (Kulia) kwenye rimoti ili kusongeza kipengee kwenye upande unayopendelea, na kisha ubonyeze kitufe cha (Weka) kwenye rimoti.
  • Unaweza kubadilishia hadi upeperushaji wa TV kwa kubonyeza tu kitufe cha TV kwenye rimoti.

Kubadilisha kutoka Menyu ya Mwanzo

  1. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague chanzo cha ingizo kutoka [Vifaa vya kuingiza data].