Kutumia mwongozo wa vipindi
Unaweza kupata kwa haraka vipindi vyako unavyopendelea.
- Bonyeza kitufe cha GUIDE ili uonyeshe mwongozo wa vipindi wa dijitali.
- Chagua kipindi cha kutazama.
Maelezo ya kipindi yanaonyeshwa. - Chagua [Angalia] ili utazame kipindi.
Ili kubadilisha mwongozo wa vipindi
Unaweza kubadilisha mwongozo wa vipindi hadi kwa [Uteuzi wa Runinga] au [Guide wa Aina]. Huenda baadhi ya machaguo yasipatikane kulingana na modeli/eneo/nchi yako. Unaweza pia kubadilisha mwongozo wa vipindi ili uone [Orodha ya Kichwa Iliyotekodiwa] (modeli za kurekodi USB HDD pekee) au [Orodha ya Kipima Saa].
- Sogeza uangazishaji hadi kushoto kwa kipengee, kisha usonge kushoto hadi ufungue menyu.
- Chagua mwongozo au orodha ya vipindi unayotaka.
Kutumia vitendaji vya hiara
- Wakati mwongozo wa vipindi unapoonyeshwa, bonyeza kitufe cha ACTION MENU na kisha uchague kipengee unachotaka.