Chapisha

Kutumia huduma jumuishi za utangazaji za TV

Kuonyesha maelezo ya maandishi

Unaweza kuona taarifa ya mchoro yenye msingi wa maandishi, ikijumuisha habari za kitaifa, taarifa ya hali ya hewa na ratiba za TV. Unaweza kuvinjari maelezo ambayo yanakupendeza, na kisha uchague ni maelezo gani unayotaka yaonyeshwe kwa kuweka nambari.

  1. Bonyeza kitufe cha (Maandishi) ili uonyeshe maelezo ya maandishi.

Kuhusu Huduma ya Maelezo ya Maandishi ya Dijitali

Huduma ya maandishi ya dijitali hutoa maudhui tondoti yenye michoro na taswira laini. Vipengele mbalimbali vinapatikana, kama vile viungo vya ukurasa na uelekezaji ambao ni rahisi kutumia. Huduma inakubaliwa na watangazaji kadhaa. (Upatikanaji wa kipengele hiki hutegemea modeli/eneo/nchi yako.)

Kuhusu Huduma ya Programu tumizi Ingiliani ya Dijitali

Huduma ya programu tumizi ingiliani hutoa maandishi na michoro ya ubora wa juu, pamoja na chaguo mahiri. Huduma inakubaliwa na watangazaji. (Upatikanaji wa kipengele hiki hutegemea modeli/eneo/nchi yako.)

Kumbuka

  • Huduma ingiliani inapatikana tu ikiwa inatolewa na mtangazaji.
  • Vitendaji vinavyopatikana na maudhui ya skrini hutofautiana kulingana na mtangazaji.
  • Ikiwa vichwa vidogo vimechaguliwa na uzindue programu ya maandishi ya dijitali kupitia kitufe cha (Maandishi) huenda vichwa vidogo, chini ya hali fulani, zikakosa kuonyeshwa. Wakati unapotoka kwenye programu ya maandishi ya dijitaji, onyesho la vichwa vidogo vitaendelea kiotomatiki.