Kutazama TV katika 3D (modeli za 3D tu)
Teua kwenye maandishi ili uruke hadi kwenye skrini husika ya mipangilio.
Modeli za 3D zina [Mipangilio ya 3D] katika [Mipangilio] — [Onyesha].
Unaweza kuzoea burudani nzito ya 3D, kama vile michezo ya 3D ya stirioskopiki na Diski za 3D za Blu-ray.
Ili utazame katika 3D, unganisha kifaa kinaingiana na 3D moja kwa moja kwenye TV kwa kutumia kebo iliyoidhinishwa ya HIGH SPEED HDMI yenye nembo ya HDMI.
- Andaa Miwani ya 3D.
- Onyesha maudhui ya 3D kwenye skrini ya TV.
- Vaa Miwani ya 3D.
Unaweza sasa kutaza picha za 3D. Ikiwa hakuna athari ya 3D itakayofikiwa, tekeleza hatua zifuatazo. - Bonyeza kitufe cha ACTION MENU, kisha uchague [3D].
- Chagua [Onyesho la 3D] ili kufaa maudhui yaliyoonyeshwa. Kulingana na mitambo au mfumo wa ingizo, huenda, [3D (Kando‑kwa‑Kando)]/[3D (Juu-Chini)] isiweze kuteulika.
Kidokezo
Kumbuka
- Athari ya 3D au inaweza kutokea sana ikiwa kipimo cha hali joto ni cha chini.
- Ikiwa [Motionflow] katika [Picha] imewekwa kuwa kitu kingine kando na [Zima], mchakato wa kupunguza kumemeka kwa skrini unaweza kuathiri mwenendo laini wa picha. Katika hali hii, bonyeza kitufe cha ACTION MENU kisha uteue [Picha] — [Mipangilio bora] — [Motionflow] — [Zima]. (Kwa modeli zinazokubaliwa na [Motionflow] pekee.)
[Motionflow] modeli zinazotangamana zina [Motionflow] katika [Mipangilio] — [Onyesha] — [Picha] — [Mipangilio bora] — [Mwendo].