Chapisha

Maelezo kuhusu kutumia kifaa cha USB HDD kurekodi (modeli za kurekodi za USB HDD tu)

Modeli za kurekodi USB HDD zina [Usanidi wa kifaa cha kurekodi] katika [Mipangilio].

  • Lazima kifaa cha USB HDD kitumiwe kwa kurekodi peke yake. Tumia kifaa tofauti cha USB HDD kutazama picha na video.
  • Kitendaji hiki kinapatikana tu kwenye baadhi ya modeli barani Ulaya, Australia na nchini Nyuzilandi.
  • USB HDD kubwa zaidi ya GB 32 tu ndizo zinazokubaliwa.
  • Muunganisho wa kifaa cha USB HDD kupitia kituo cha USB haukubaliwi. Unganisha kifaa moja kwa moja kwa TV.
  • Data yoyote iliyohifadhiwa katika kifaa cha USB HDD itafutwa ikiwekwa upya wakati wa mchakato wa usajili. Kifaa cha USB HDD hakiwezi kutumiwa na Kompyuta wakati kimesajiliwa kwenye TV. Ili kuwezesha kifaa cha USB HDD kwenye Kompyuta, kiweke upya kwenye Kompyuta. (Kumbuka kwamba data yoyote katika kifaa cha USB HDD itafutwa.)
  • Vifaa visivyozidi 8 vya USB HDD vinaweza kusajiliwa.
  • TV hii tu ndiyo itakayoweza kucheza data iliyorekodiwa kwenye USB HDD ambayo imesajiliwa kwenye TV hii.
  • Rekodi inakubaliwa tu kwa matanganzo ya TV na redio za dijitali. Kurekodi matangazo ya data hakukubaliwi.
  • Mawimbi yaliyoharibika/kusimbwa hayawezi kurekodiwa.
  • Kurekodi hakuwezi kutekelezwa katika hali zifuatazo:
    • TV haiwezi kutambua kifaa kilichosajiliwa cha USB HDD.
    • Zaidi ya vipindi 1,000 vimerekodiwa kwenye kifaa cha USB HDD.
    • Kifaa cha USB HDD kimejaa.
  • Huenda uteuzi otomati wa kipindi usiwezekane wakati kinaporekodiwa.
  • Kurekodi kipindi hakuwezekani isipokuwa rekodi hiyo imeidhinishwa.
  • Ikiwa TV imegongeshwa wakati wa kurekodi USB HDD, huenda kelele ikatokea katika maudhui yaliyorekodiwa.
  • Hakuna wakati wowote Sony itawajibika kwa kushindwa kurekodi au uharibifu au upotezaji wowote wa maudhui yaliyorekodiwa au yanayohusishwa na kuharibika kwa TV, mwingiliano wa ishara, au tatizo jingine lolote.