Chapisha

Kutazama/kufuta maudhui yaliyorekodiwa (modeli za kurekodi za USB HDD tu)

Modeli za kurekodi USB HDD zina [Usanidi wa kifaa cha kurekodi] katika [Mipangilio].

Kumbuka

  • Kitendaji hiki kinapatikana tu kwenye baadhi ya modeli barani Ulaya, Australia na nchini Nyuzilandi.

Kutazama maudhui yaliyorekodiwa

  1. Bonyeza kitufe cha TITLE LIST, kisha uteue maudhui ya kutazamwa.

Kufuta maudhui yaliyorekodiwa

  1. Bonyeza kitufe cha TITLE LIST.
    Ikiwa rimoti iliyonunuliwa haina kitufe cha TITLE LIST, teua (ikoni ya Programu) kwenye Menyu ya nyumbani na uteue [Orodha ya Kichwa Iliyotekodiwa] kwenye orodha ya programu.
  2. Bonyeza kitufe cha ACTION MENU, na uteue yafuatayo kwa utaratibu.
    [Futa] — kipindi cha kufuta — [Futa]
    Ili kufuta vipindi anuwai, chagua vipindi vyote unavyotaka kufuta kabla ya kuchagua [Futa].

Kwa maelezo kuhusu maana ya ishara zilizo katika orodha ya vichwa vilivyorekodiwa, angalia Kuelewa alama zilizoonyeshwa kwenye orodha iliyorekodiwa ya majina (modeli za kurekodi USB HDD pekee).