Chapisha

Maelezo kuhusu vifaa vya USB vilivyotumiwa kuhifadhi picha na muziki

  • Vituo vya USB kwenye TV hukubali mifumo ya faili ya FAT16, FAT32, exFAT, na NTFS.
  • Wakati unapounganisha kamera ya picha tulivu ya Sony kwa TV kwa kutumia kebo ya USB, mipangilio ya muunganisho wa USB kwenye kamera yako inahitaji kuwekwa hali ya “Oto” au ya “Kihifadhi vitu vingi”.
  • Kama kamera yako tuli ya dijitali haifanyi kazi na TV yako, jaribu yafuatayo:
    • Weka mipangilio ya muunganisho wa USB kwenye kamera yako kuwa “Kihifadhi vitu vingi”.
    • Nakili faili kutoka kwenye kamera hadi kwenye hifadhi ya USB, kisha unganisha hifadhi kwenye TV.
  • Baadhi ya picha na filamu zinaweza kukuzwa na kusababisha ubora wa chini wa picha. Kulingana na ukubwa na uwiano wa mgao, huenda picha zikaonyeshwa katika skrini nzima.
  • Huenda ikachukua muda mrefu kuonyesha picha, kulingana na faili au mipangilio.
  • Hakuna wakati wowote Sony itawajibika kwa kushindwa kurekodi au uharibifu au upotezaji wowote wa maudhui yaliyorekodiwa au yanayohusishwa na kuharibika kwa runinga, kuharibika kwa kifaa cha USB, au tatizo lingine lolote.