Kuunganisha Blu-ray au kichezaji cha DVD
Unganisha kichezaji cha Blu-ray/DVD kwenye TV.
Tumia mbinu ya muunganisho iliyo hapa chini kulingana na temino zinazopatikana kwenye TV yako.
Kumbuka
- Temino zinazopatikana hutegemea modeli/eneo/nchi yako.
Kidokezo
- Unaweza pia kuunganisha king'amuzi (kisanduku cha kebo/satelaiti) kwa njia sawa na kichezaji cha Blu-ray/DVD.
Muunganisho wa HDMI
Kwa picha zenye ubora wa juu zaidi, tunapendekeza uunganishe kichezaji chako kwenye TV kwa kutumia kebo ya HDMI. Ikiwa kichezaji chako cha Blu-ray/DVD kina jaki (soketi) ya HDMI, iunganishe kwa kutumia kebo ya HDMI.
- Kichezaji cha Blu-ray/DVD (sawa na kuunganisha king'amuzi)
- Kebo ya HDMI (haijapeanwa)*
* Hakikisha unatumia kebo iliyoidhinishwa ya HIGH SPEED HDMI yenye nembo ya HDMI.
- Ikiwa kifaa kina jeki ya DVI (soketi), kiunganishe kwenye kituo cha HDMI (yenye AUDIO IN) kupitia kiolesura cha adapta cha DVI - HDMI (haijatolewa), na unganisha jeki (soketi) za kutoa sauti za kifaa kwa HDMI 3 AUDIO IN / HDMI 1 AUDIO IN.
Upatikanaji wa kipengele hiki unategemea modeli/eneo/nchi yako. Rejelea Reference Guide ili ukague ikiwa TV yako inakubali HDMI 3 AUDIO IN / HDMI 1 AUDIO IN.
Muunganisho wa kijenzi cha video
Ikiwa kichezaji chako cha Blu-ray/DVD kina jeki (soketi) za kijenzi cha video, viunganishe kwenye TV kwa kutumia kebo ya kijenzi cha video na kebo ya sauti.
- Kichezaji cha Blu-ray/DVD (sawa na kuunganisha king'amuzi)
- Kebo ya video ya kijenzi (haijapeanwa)
- Kebo ya sauti (haijapeanwa)
Muunganisho sawia
Ikiwa kichezaji cha Blu-ray/DVD kina jeki sawia (soketi), iunganishe kwa kutumia kebo sawia ya video/sauti.
- Kichezaji cha Blu-ray/DVD (sawa na kuunganisha king'amuzi)
- Kebo ya video/sauti (haijapeanwa)
Unapotumia Kebo ya Kurefusha Analogi
- Kichezaji cha Blu-ray/DVD (sawa na kuunganisha king'amuzi)
- Kebo ya Kurefusha Analogi (haijapeanwa)*
- Kebo ya RCA (haijajumuishwa)
* Kupatikana kwa Kebo ya Kurefusha Analogi kunategemea modeli/eneo/chini yako.