Kuunganisha kamera au kamkoda na kuangalia maudhui yaliyohifadhiwa
Kuunganisha kamera au kamkoda
Unganisha kamera yako tuli ya dijitali ya Sony au kamkoda kwa kutumia kebo ya HDMI. Tumia kebo ambayo ina jeki ndogo ya HDMI kwa kamera tuli ya dijito/mwisho wa kamkoda, na jeki ya kawaida ya HDMI kwa mwisho wa TV.
- Kamera ya dijitali ya picha
- Kamkoda
- Kebo ya HDMI (haijapeanwa)*
* Hakikisha unatumia kebo iliyoidhinishwa ya HIGH SPEED HDMI yenye nembo ya HDMI.
Kutazama maudhui yaliyohifadhiwa kwenye kamera tuli ya dijitali/kamkoda
- Baada ya kuunganisha kamera ya picha tulivu/kamkoda ya dijitali, iwashe.
- Bonyeza kitufe cha (Weka uteuzi) mara kwa mara ili uteue kamera tuli ya dijitali/kamkoda iliyounganishwa.
- Anza kucheza kwenye kamera tuli ya dijitali iliyounganishwa/kamkoda.
Kukagua fomati za faili zinazokubaliwa
Kidokezo
- Ukiunganisha kifaa kinachoingiana na BRAVIA Sync, unaweza kukiendesha kwa kutumia rimoti ya runinga tu. Hakikisha kwamba kifaa kinatangamana na BRAVIA Sync. Vifaa vingine huenda visitangamane BRAVIA Sync ijapokuwa vina jeki ya HDMI.