Chapisha

Kuonyesha skrini ya simu maizi/kompyuta kibao kwenye TV kwa kutumia kebo ya MHL (MHL modeli zinazokubaliwa tu)

Alama ya (MHL) ipo kando ya kituo cha HDMI IN 1/MHL (modeli zinazokubali MHL 2K pekee) au kituo cha HDMI IN 2/MHL (modeli zinazobali MHL 4K pekee).

Kuunganisha kifaa cha mkononi na towe ya MHL

Kwa modeli za 2K, unganisha kifaa chako cha mkononi kwenye kituo cha TV cha HDMI IN 1/MHL, kwa kutumia kebo ya MHL.

Kwa modeli za 4K, unganisha kifaa chako cha mkononi kwenye kituo cha TV cha HDMI IN 2/MHL, kwa kutumia kebo ya MHL.

Illustration of the connection method
  1. MHL kifaa cha mkononi
  2. Kebo ya MHL (haijapeanwa)*

* Kwa ishara za 2K, hakikisha kutumia MHL iliyoidhinishwa ya kebo 2 yenye nembo ya MHL.
Kwa modeli za 4K, hakikisha kutumia MHL iliyoidhinishwa ya kebo 3 zenye nembo ya MHL. Ikiwa kifaa chako cha mkononi cha MHL kinakubali towe ya 4K, tumia MHL iliyoidhinishwa ya kebo 3.

Kuona maudhui yaliyohifadhiwa katika kifaa cha mkononi na towe ya MHL

  1. Baada ya kuunganisha kifaa chako cha mkononi, bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue ingizo ambalo kifaa chako cha mkononi kimeunganishwa.

Kubadilisha ingizo la MHL kiotomatiki

  1. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Ingizo za nje] — [Mipangilio ya BRAVIA Sync] — [Badiliko la ingizo oto (MHL)] — [Washa]. (Kulingana na kifaa cha mkononi, ingizo huenda isikabadilishe kiotomatiki.) Ikiwa TV iko katika hali ya kusubiri, haitabadilisha kiotomatiki.

Kuchaji kifaa cha mkononi

Wakati TV imewashwa, TV inaweza kuchaji kifaa cha mkononi ikiwa imeunganishwa kwa kutumia kebo ya MHL.

Kumbuka

  • Simu maizi/kompyuta kibao pekee zinazokubali MHL zinaweza kutumia kipengele hiki.

Kidokezo

Ikiwa [Kuchaji kwa MHL wakati wa kusubiri] imewekwa kuwa [Washa], TV inaweza kuchaji kifaa cha MHL wakati TV iko katika hali ya kusubiri.

Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Ingizo za nje] — [Mipangilio ya BRAVIA Sync] — [Kuchaji kwa MHL wakati wa kusubiri] — [Washa].