Chapisha

Kutumia Wi-Fi Direct kuunganisha kwenye TV (hakuna kipanga njia pasiwaya kinachohitajika)

Unaweza kuunganisha kifaa kwenye TV pasiwaya, bila kutumia kipanga njia pasiwaya, na kisha utiririshe video, picha, na muziki ambao umehifadhiwa kwenye kifaa chako moja kwa moja kwenye TV.

Illustration of content streaming
  1. Bonyeza kitufe cha HOME kisha uteue, [Mipangilio] — [Mtandao] — [Wi‑Fi Direct] — [Mipangilio ya Wi‑Fi Direct].
  2. Chagua jina la TV lililoonyeshwa kwenye skrini ya TV na kifaa cha Wi-Fi Direct.
    Ikiwa kifaa hakikubali Wi-Fi Direct, chagua [Onyesha Mtandao (SSID)/Nenosiri].
  3. Tumia kifaa cha Wi-Fi Direct/Wi-Fi ili kuunganisha na TV.
  4. Tuma maudhui kutoka kwenye kifaa cha Wi-Fi Direct/Wi-Fi kwenye TV.
    Kwa maelezo, rejelea mwongozo wa maagizo wa kifaa.

Usipofanikiwa kuunganisha

Wakati skrini ya kusubiri ya mpangilio wa Wi-Fi Direct imeonyeshwa, chagua, [Onyesha Mtandao (SSID)/Nenosiri] na ufuate maagizo kwenye skrini ili ukamilishe usanidi.

Ili kuunganisha kifaa kingine

Fuata hatua hapo juu ili kuunganisha vifaa. Hadi vifaa 10 vinaweza kuunganishwa kwa wakati mmoja. Ili kuunganisha kifaa kingine wakati vifaa 10 vimeunganishwa tayari, tenganisha kifaa kisichofaa, kisha unganisha kifaa kingine.

Ili kubadilisha jina la TV lililoonyeshwa kwenye kifaa kilichounganishwa

Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Kuhusu] — [Jina la kifaa].

Ili kuorodhesha vifaa vilivyounganishwa/batilisha usajili wa vifaa

Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Mtandao] — [Wi‑Fi Direct] — [Onyesha orodha ya kifaa/Futa].

Ili ubadilishe usajili wa kifaa, chagua kifaa katika orodha ili kufuta, kisha ubonyeze kitufe cha (Weka). Kisha, chagua [Ndiyo] katika skrini ya uthibitishaji.

Ili kubadilisha usajili wa vifaa vyote, chagua [Futa Zote] katika orodha, kisha [Ndiyo] katika onyesho la udhibitisho.