Kurekebisha mipangilio ya mtandao wa nyumbani
Teua kwenye maandishi ili uruke hadi kwenye skrini husika ya mipangilio.
Unaweza kurekebisha mipangilio ya mtandao wa nyumbani.
Kukagua muunganisho wa seva
Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Mtandao] — [Uwekaji wa mtandao wa nyumbani] — [Uchunguzi wa seva] — fuata maagizo kwenye skrini ili utekeleze utambuzi.
Kutumia kitendaji cha kitungulizaji
Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Mtandao] — [Uwekaji wa mtandao wa nyumbani] — [Renderer] — chaguo unalotaka.
- [Dhima ya Renderer]
- Wezesha kitendaji cha kitungulizaji
- Unaweza kucheza faili za picha/muziki/video katika kidhibiti (k.v., kamera ya dijitali) kwenye skrini ya TV kwa kutumia kifaa moja kwa moja.
- [Udhibiti wa kufikia Renderer]
- Chagua [Idhini Otomatiki ya Ufikivu] ili ufikie TV kiotomatiki wakati kidhibiti kinapofikia TV kwa mara ya kwanza.
- Teua [Mipangilio Kaida] ili ubadilishe mipangilio ya kibali cha ufikiaji cha kila kidhibiti.
Kutumia kifaa cha mbali
Bonyeza kitufe cha HOME, kischa uteue [Mipangilio] — [Mtandao] — [Mipangilio ya kifaa cha mbali] — chaguo unalotaka.
- [Dhibiti kutoka mbali]
- Wezesha matumizi ya TV kutoka kwenye kifaa kilichosajiliwa.
- [Batilisha usajili wa kifaa cha mbali]
- Badilisha usajili wa kifaa ili ulemaze matumizi ya TV kutoka kwenye kifaa hicho.