Kuunganisha kwenye mtandao kwa kutumia kebo ya LAN
Teua kwenye maandishi ili uruke hadi kwenye skrini husika ya mipangilio.
Kuunganisha kwenye mtandao kwa kutumia kebo ya LAN
Muunganisho wa LAN wenye waya hukuwezesha kufikia Wavuti na mtandao wako wa nyumbani.
Hakikisha umeunganishwa kwenye Intaneti au mtandao wa nyumbani kupitia kipanga njia.
Kidokezo
- Ikiwa unatumia modemu chenye vitendaji vya kipanga njia, hupaswi kuandaa kipanga njia tofauti. Muulize mtoa huduma wako kwa maelezo kuhusu sifa za modemu yako.
- Kebo ya LAN
- Kompyuta
- Kipanga njia
- Modemu
- Intaneti
- Sanidi kipanga njia chako cha LAN.
Kwa maelezo zaidi, rejelea mwongozo wa maagizo wa kipanga njia chako cha LAN, au wasiliana na mtu aliyesanidi mtandao (msimamizi wa mtandao). - Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Mtandao] — [Usanidi wa mtandao] — [Rahisi].
- Fuata maagizo ya kwenye skrini ili ukamilishe usanidi.
Kumbuka
- Mipangilio inayohusiana na mtandao ambayo inahitaji huenda ikatofautiana kulingana na mtoa huduma wa Intaneti au kipanga njia. Kwa maelezo, rejelea miongozo ya maagizo inayotolewa na mtoa huduma ya Wavuti, au zile zinazotolewa na kipanga njia. Au wasiliana na mtu anayesanidi mtandao (msimamizi wa mtandao).