Chapisha

Kuweka kipima saa

Kuweka kipima saa cha kuwasha

Kipima saa cha kuwasha huwasha TV kiotomatiki kwa wakati fulani, kama wakati kipindi unachotaka kukitazama kinapoanza. Hukuwezesha pia kutumia TV kama saa ya kengele.

  1. Bonyeza kitufe cha HOME, na uteue (ikoni ya Saa) — [Kipima saa c. Kuwasha] — chaguo unalotaka.

Kuweka kipima saa cha kulala

Kipima saa cha kulala huzima TV kiotomatiki baada ya muda uliowekwa mapema.

  1. Bonyeza kitufe cha HOME, na uteue (ikoni ya Saa) — [Kilalishaji cha Majira] — chaguo unalotaka.

Kumbuka

  • Wakati unapozima TV, na kuiwasha tena, [Kilalishaji cha Majira] huwekwa upya kwa [Zima].