Kifaa cha nje (kama vile kisanduku cha kusanidi au kipokeaji cha AV) hakiwezi kudhibitiwa kupitia IR Blaster. (Kwa modeli zinazokubaliwa na IR Blaster pekee)
Teua kwenye maandishi ili uruke hadi kwenye skrini husika ya mipangilio.
Modeli zinazotangamana na IR Blaster zina [Usanidi wa IR Blaster] katika [Mipangilio] — [Ingizo za nje].
- Hakikisha kwamba IR Blaster imesanidiwa vizuri na kipitisha IR kiko karibu na kipokea IR cha kifaa cha nje.
- Hakikisha kwamba TV yako inakubali kifaa cha nje.
- Ukibonyeza na ushikilie kitufe kwenye rimoti, huenda shughuli isifanye kazi. Badala yake, jaribu kubonyeza kitufe kwa kurudia.
- Baadhi ya vifaa vya nje huenda visikaitikie baadhi ya vitufe kwenye “Menyu ya Kitendo”.
- Huenda IR Blaster haijawekwa vizuri. Ili kusanidi IR Blaster, bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Ingizo za nje] — [Usanidi wa IR Blaster].