Kutazama/kufuta maudhui yaliyorekodiwa (modeli za kurekodi za USB HDD tu)
Teua kwenye maandishi ili uruke hadi kwenye skrini husika ya mpangilio.
Modeli za kurekodi USB HDD zina [Usanidi wa kifaa cha kurekodi] katika [Mipangilio] — [Kutazama runinga].
Kumbuka
- Kitendaji hiki kinapatikana tu kwenye baadhi ya modeli barani Ulaya, Australia na nchini Nyuzilandi.
Kutazama maudhui yaliyorekodiwa
- Bonyeza kitufe cha TITLE LIST kisha uchague maudhui ya kutazamwa.
Kufuta maudhui yaliyorekodiwa
- Bonyeza kitufe cha TITLE LIST.
- Bonyeza kitufe cha ACTION MENU, na uchague yafuatayo kwa utaratibu.
[Futa] — kipindi cha ili kufuta — [Futa]
Ili kufuta vipindi vingi, teua vpindi vyote unavyotaka kufuta kabla ya kuteua [Futa].
Kwa maelezo kuhusu maana ya ishara zilizo katika orodha ya vichwa vilivyorekodiwa, angalia Kuelewa alama zilizoonyeshwa kwenye orodha iliyorekodiwa ya majina (modeli za kurekodi USB HDD pekee).