Chapisha

Kucheza maudhui kutoka kwenye kompyuta

Unaweza kufurahia maudhui (faili za picha/muziki/video) yaliyohifadhiwa kwenye kifaa cha mtandao kilicho katika chumba kingine, ukiunganisha TV kwa mtandao wa nyumbani kupitia kipanga njia.

Illustration of the connection method
  1. Kompyuta (seva)
  2. Kipanga njia
  3. Modemu
  4. Intaneti
  1. Unganisha TV kwenye mtandao wako wa nyumbani.
  2. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague (aikoni ya Programu) kutoka kwenye Menyu ya mwanzo, kisha uchague [Kicheza Media].
    Ikiwa rimoti iliyokuja nayo ina kitufe cha APPS, unaweza kubonyeza kitufe cha APPS.
  3. Chagua jina la kifaa cha mtandao.
  4. Chagua folda, na kisha uchague faili ya kucheza.

Kukagua fomati za faili zinazokubaliwa

Kumbuka

  • Kulingana na faili, uchezaji huenda usiwezekane hata wakati wa kutumia fomati zinazokubaliwa.