Chapisha

Kurekebisha mipangilio ya BRAVIA Sync

  1. Washa kifaa kilichounganishwa.
  2. Ili kuwezesha [Udhibiti wa BRAVIA Sync], bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Kutazama runinga] — [Ingizo za nje] — [Mipangilio ya BRAVIA Sync] — [Udhibiti wa BRAVIA Sync].
  3. Wezesha BRAVIA Sync kwenye kifaa kilichounganishwa.
    Wakati kifaa maalum kinachotangamana na Sony BRAVIA Synckimeunganisha na kuwashwa na [Udhibiti wa BRAVIA Sync] imewezeshwa, BRAVIA Sync huwezeshwa kiotomati kwenye kifaa hicho. Kwa maelezo, rejelea mwongozo wa maagizo wa kifaa kilichounganishwa.

Chaguo zinazopatikana

Chaguo zinazopatikana huonyeshwa hapa chini. (Chaguo hutofautiana kulingana na modeli/eneo/nchi yako.)

[Uzimaji oto wa vifaa]
Ikilemazwa, kifaa kilichounganishwa hakizimwi kiotomatiki wakati TV imezimwa.
[Uwashaji oto wa Runinga]
Ikilemazwa, TV haiwaki kiotomatiki wakati kifaa kilichounganishwa kimewashwa.
[Orodha ya kifaa cha BRAVIA Sync]
Huonyesha orodha ya vifaa vya BRAVIA Sync.
[Funguo za kudhibiti kifaa]
Hukuruhusu uweke vitufe vya kudhibiti kifaa kilichounganishwa cha HDMI.

Ili utumie Menyu landanifu

  1. Bonyeza kitufe cha ACTION MENU, chagua Menyu landanifu, na uchague kipengee unachotaka katika Menyu landanifu.

Kidokezo

  • Katika masuala yafuatayo, ujumbe hutokea kwenye skrini ya TV unapochagua Menyu landanifu.
    • Kifaa cha HDMI hakijaunganishwa.
    • [Udhibiti wa BRAVIA Sync] imelemazwa.