Chapisha

Kurekebisha mpangilio wa ulandanishi wa AV

Ikiwa kifaa cha sauti cha Bluetooth kimeunganishwa, huenda kukawa na kuchelewa kati ya picha na sauti kwa sababu ya sifa za Bluetooth. Unaweza kurekebisha kuchelewa kati ya picha na sauti kwa kutumia mpangilio wa Mlandanisho wa A/V. (Ni za modeli zinazokubali Bluetooth A2DP pekee ndizo ambazo zinaweza kutumia vifaa vya sauti vya Bluetooth.)

Modeli zinazokubali Bluetooth A2DP ambazo hutumia vifaa vya sauti vya Bluetooth ndizo zina [Mlandanisho wa A/V] katika [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Zao la sauti].

  1. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Zao la sauti] — [Mlandanisho wa A/V] — chaguo unalotaka.

Kidokezo

  • Unaweza pia kurekebisha muda wa utoaji wa picha na sauti ikiwa mfumo maalum wa sauti umeunganishwa na kebo ya HDMI. Kwa maelezo kuhusu modeli zinazokubaliwa, rejelea tovuti ya usaidizi.

Kumbuka

  • Kulingana na kifaa kilichouganishwa cha sauti cha Bluetooth, huenda picha na sauti zisilingane hata wakati mpangilio wa [Mlandanisho wa A/V] umewekwa kwa [Washa] au [Oto].
  • Ili kuzuia TV dhidi ya kuonyesha skrini nyeusi mara moja baada ya kuiwasha wakati mwambaa wa sauti umeunganishwa pasi waya (Bluetooth) weka mpangilio wa [Mlandanisho wa A/V] kwa [Washa].
  • Ikiwa [Modi ya Picha] imewekwa kwa moja ya chaguo hapa chini, muda towe wa picha na sauti haurekebishwi hata wakati mpangilio wa [Mlandanisho wa A/V] umewekwa kwa [Oto].
    • [Mchezo]
    • [Michoro]
    • [Picha‑Nga'vu]
    • [Picha‑Wastani]
    • [Picha‑Kukaida]
    Ili urekebishe [Mlandanisho wa A/V] ukiwa katika modi yoyote kati ya hizi, chagua [Washa].
  • Uwezo wa TV kuitikia wakati unacheza michezo ya video unaweza kuwa wa polepole kwa sababu ya mpangilio wa [Mlandanisho wa A/V] unaongeza kuchelewa kwenye muda towe wa picha. Kwa michezo ambayo inategemea kasi ya mwitikio, hatupendekezi utumie kifaa cha Bluetooth na tunapendekeza kwamba utumie spika za TV au mwambaa wa sauti wenye muunganisho wa waya (kebo yaHDMI /kebo ya optiki ya dijitali) badala yake.