Chapisha

Kuunganisha IR Blaster (modeli zinazoingiana na IR Blaster pekee)

Modeli zinazotangamana na IR Blaster zina [Usanidi wa IR Blaster] katika [Mipangilio] — [Kutazama runinga] — [Ingizo za nje].

IR Blaster hukuwezesha kutumia kisanduku cha set-top (kisanduku cha kebo/satelaiti) ambacho kimeunganishwa kwenye TV, kwa kutumia rimoti ya TV.

(Huenda modeli zinazotangamana za IR Blaster zisipatikane kulingana na modeli/nchi yako.)

Illustration of the connection method
  1. Kisanduku cha set-top (kisanduku cha kebo/satelaiti)
  2. Kebo ya IR Blaster
  3. Jeki ya IR Blaster (soketi)

Kumbuka

  • Hakikisha kwamba IR Blaster imesanidiwa vizuri na kipitisha IR kiko karibu na kipokea IR cha kifaa cha nje.
  • Hakikisha kwamba TV yako inakubali kifaa cha nje.