Chapisha

[Mipangilio ya paneli ya kitaalam] (kwa modeli zilizo na paneli ya OLED pekee)

Chaguo hizi zinapatikana kwa modeli zenye paneli ya OLED na hutumika kuzuia kubakia kwa picha.

Ikiwa picha ile moja imeonyeshwa kwa kurudia au kwa kipindi cha muda mrefu, picha inaweza kubakia.
TV hii ina vitendaji viwili, [Ubadilishaji pikseli] na [Onyesha Paneli upya], ambavyo vimeundwa kupunguza kubakia kwa picha.

Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Mipangilio ya paneli ya kitaalam] — chaguo unalotaka.

Chaguo zinazopatikana

[Ubadilishaji pikseli]
Husogeza picha iliyoonyeshwa kwa wakati tofauti ili kuzuia picha kubakia. Katika hali za kawaida, tumia TV chaguo hili likiwa limewezeshwa.
[Onyesha Paneli upya]
Tekeleza kwa mkono uonyeshaji paneli upya wakati ubakiaji wa picha unapoonekana sana tu.

Kumbuka

  • Tekeleza uonyeshaji paneli upya wakati ubakiaji wa picha unaonekana sana tu. Kama rejeo, tekeleza hatua hii mara moja kwa mwaka. Epuka kuitekeleza zaidi ya mwaka moja kwa mwaka kwa sababu inaweza kuathiri maisha ya matumizi ya paneli.
  • Kuonyesha paneli upya huchukua karibu saa moja kukamilika. Huenda mstari mweupe ukaonekana kwenye skrini wakati wa kuonyesha paneli upya. Hii sio dosari ya TV.
  • Tekeleza marekebisho wakati halijoto ya chumba ni kati ya 10°C na 40°C. Ikiwa halijoto ya chumba ni nje ya masafa haya, huenda kuonyesha paneli upya kusikamilike.