Chapisha

Kutumia maikrofoni inayodhibitiwa na rimoti

Rimoti ambazo zinakubali Utafutaji wa Sauti zina kitufe cha Maikrofoni na maikrofoni iliyoundiwa ndani. Kwa kuongea kwenye maikrofoni, unaweza kutafuta maudhui mbalimbali.

  1. Bonyeza kitufe cha Maikrofoni.

    LED kwenye rimoti itawaka.

  2. Ongea kwenye maikrofoni.

    Mifano ya usemi inaweza kuonyeshwa kulingana na modeli yako.

    Kielelezo cha kuzungumza kwenye sehemu ya juu ya kidhibiti cha mbali

    Matokeo ya utafutaji huonyeshwa wakati unaongea kwenye maikrofoni.

Kidokezo

  • Kulingana na matokeo ya utafutaji, ukibonyeza juu kwenye rimoti, matokeo zaidi ya utafutaji yataonyeshwa. Mfano wa picha ya skrini wakati kuna matokeo zaidi ya utafutaji

Wakati huwezi kutafuta kwa kutumia sauti

Sajili rimoti ya sauti ambayo ina kitufe cha Maikrofoni kwenye TV tena kwa kubonyeza kitufe cha HOME na kuchagua [Mipangilio] — [Kiungambali na Vifaa vya Ziada] — [Udhibiti mbali] — [Unganisha kupitia Bluetooth].

Kumbuka

  • Muunganisho wa Intaneti na akaunti ya Google vinahitajika ili utumie Kutafuta kwa Kutamka.
  • Aina ya rimoti inayotolewa pamoja na TV, na upatikanaji wa rimoti yenye maikrofoni iliyoundiwa ndani hutofautiana kulingana na modeli/eneo/nchi yako. Rimoti ya hiari inapatikana katika baadhi ya modeli/maeneo/nchi.