Chapisha

Vipengele vya ufikiaji

TV hii ina vipengele vya ufikiaji katika [Ufikiaji] kama vile kipengee cha maandishi hadi matamshi kwa maandisi ya kwenye skrini, kukuza ili kurahisisha kusoma na manukuu/maelezo mafupi.

Bonyeza kitufe cha HOME, kischa uchague [Mipangilio] — [Mapendeleo ya Kifaa] — [Ufikiaji] ili usanidi vipengele vya kumsaidia mtumiaji.

[Ufikiaji] ina kitendaji cha njia ya mkato ili uweze kukiwasha au kukizima kwa kubonyeza na kushikilia kitufe cha AUDIO kwenye rimoti kwa sekunde 3.

Kidokezo

  • Mpangilio msingi wa kitendaji ambacho hufanya kazi unapobonyeza na kushikilia kitufe cha AUDIO kwenye rimoti kwa sekunde 3 ni [Talkback]. Wezesha kitendaji kwa kutumia [Njia mkato ya ufikiaji] katika [Ufikiaji], na ubadilishe kipengele kilichoteuliwa kwa kutumia [Huduma ya njia ya mkato].
  • Ili utumie ubadilishaji wa matini kuwa usemi kwenye Mwongozo wa Usaidizi, tazama Mwongozo wa Usaidizi katika tovuti ya usaidizi ya Sony kwa kutumia kompyuta au simu maizi.

    http://www.sony-asia.com/support/ Msimbo wa QR kwa tovuti ya usaidizi wa Sonyhttp://www.sony-asia.com/support/