Kuunganisha Blu-ray au kichezaji cha DVD
Unganisha kichezaji cha Blu-ray/DVD kwenye TV.
Tumia mbinu ya muunganisho iliyo hapa chini kulingana na temino zinazopatikana kwenye TV yako.
Kumbuka
- Temino zinazopatikana hutegemea modeli/eneo/nchi yako.
Kidokezo
- Unaweza pia kuunganisha king'amuzi (kisanduku cha kebo/satelaiti) kwa njia sawa na kichezaji cha Blu-ray/DVD.
Muunganisho wa HDMI
Kwa picha zenye ubora wa juu zaidi, tunapendekeza uunganishe kichezaji chako kwenye TV kwa kutumia kebo ya HDMI. Ikiwa kichezaji chako cha Blu-ray/DVD kina jaki (soketi) ya HDMI, iunganishe kwa kutumia kebo ya HDMI.
- Kichezaji cha Blu-ray/DVD (sawa na kuunganisha king'amuzi)
- Kebo ya HDMI (haijapeanwa)*
- Hakikisha unatumia kebo iliyoidhinishwa ya HIGH SPEED HDMI yenye nembo ya HDMI.
Muunganisho sawia
Ikiwa kichezaji cha Blu-ray/DVD kina jeki sawia (soketi), iunganishe kwa kutumia kebo sawia ya video/sauti.
- Kichezaji cha Blu-ray/DVD (sawa na kuunganisha king'amuzi)
- Kebo ya video/sauti (haijapeanwa)