Mipangilio mahiri ya “Sauti”
Ukurasa huu huweka mipangilio mbalimbali ya vipengele unavyoweza kusanidi katika [Sauti] — [Mahiri].
Kumbuka
- Onyesho halisi linaweza kutofautiana au baadhi ya mipangilio huenda isipatikane kulingana na modeli/nchi/eneo lako na kifaa kilichounganishwa.
[Mahiri]
| Mpangilio | Maelezo |
|---|---|
| Kawaida | Rekebisha [Kiwango Sauti Oto], [Linganisha], na [Kiwango sauti cha zao la sikizi dijitali]*.
|
| Inayohusiana na ingizo | Rekebisha [Sawazisha Sauti] na [Masafa ya elimumwendo]. |
| Weka upya | Rejesha mipangilio yote ya sauti kwa mipangilio chaguo-msingi ya kiwandani. |