Chapisha

Sasisho za programu

Sony itatoa visasisho vya programu mara kwa mara ili kuboresha matumizi na kuwapa watumiaji uzoefu mpya wa TV. Njia rahisi ya kupokea visasisho vya programu ni kupitia muunganisho wa Intaneti hadi kwenye TV.

Ikiwa unataka kuangalia ikiwa programu yako imesasishwa, teua [Sasisho la mfumo] kutoka [Mipangilio] — [Mapendeleo ya Kifaa] — [Kuhusu].

Kusasisha programu kupitia kifaa cha hifadhi cha USB

Ikiwa huna muunganisho wa mtandao, unaweza pia kusasisha programu kwa kutumia kifaa cha hifadhi cha USB. Tumia kompyuta yako kupakua programu mpya kutoka kwenye tovuti ya usaidizi ya Sony kwenye kifaa cha kuhifadhi cha USB. Weka kifaa cha kuhifadhi cha USB kwenye kituo cha USB hadi kwenye TV na usasishaji wa programu utaanza kiotomatiki.

Ikiwa utasasisha programu ya TV kwa kutumia kifaa cha hifadhi cha USB, unastahili kusoma tahadhari za kusasisha kwa kutumia kifaa cha hifadhi cha USB kwenye tovuti.

Kwa maelezo zaidi kuhusu tovuti ya usaidizi, tafadhali tazama ukurasa wa Tovuti ya Msaada.