Kuna kelele ya picha au sauti wakati wa kutazama kituo cha TV cha analogi.
- Hakikisha kwamba antena (kinasa mawimbi) imeunganishwa kwa kutumia kebo ya coaxial ya 75-ohm ya ubora wa juu.
- Weka kebo ya antena (kinasa mawimbi) mbali na kebo nyingine zinazounganisha.
- Kagua mipangilio ya [Uwekaji kabla wa programu mwenyewe].
Upatikanaji wa [Uwekaji kabla wa programu mwenyewe] unatofautiana kutegemea eneo/nchi.
Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Mipangilio ya BRAVIA] — [Usanidi wa Idhaa] — [Uwekaji wa analogi] — [Uwekaji kabla wa programu mwenyewe].
- Fanya [AFT] ili upate picha na sauti bora zaidi.
- Weka [Kichujio cha Sauti] kwa [Zima], [Chini] au [Juu] ili uboreshe mapokezi ya analogi.