Chapisha

Hakuna sauti au sauti iko chini kwenye mfumo wa sauti wa nyumbani.

  • Bonyeza kitufe cha (Mipangilio ya Haraka), kisha uchague [Vipaza sauti] — [Mfumo wa sikizi].
  • Kama mfumo wa sauti hautangamani na Dolby Digital au DTS, weka [Mipangilio] — [Mipangilio ya BRAVIA] — [Zao la sauti dijito] kwenye [PCM].
  • Ukichagua kituo cha analogi (RF) na picha hazionyeshwi vizuri, badilisha mfumo wa matangazo ya TV. Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Mipangilio ya BRAVIA] — [Usanidi wa Idhaa] — [Uwekaji wa analogi] — [Uwekaji kabla wa programu mwenyewe] — [Mfumo wa Runinga]. (Upatikanaji wa [Uwekaji kabla wa programu mwenyewe] unatofautiana kutegemea eneo/nchi.)
  • Kagua ikiwa mipangilio wa [Kiwango sauti cha zao la sikizi dijitali] ya TV imewekwa kiwango cha juu zaidi.

    Bonyeza kitufe cha (Mipangilio ya Haraka), kisha uchague [Mipangilio ya sauti] — [Mahiri] — [Kawaida] — [Kiwango sauti cha zao la sikizi dijitali].

  • Wakati unatumia ingizo la HDMI lenye Sauti Murua ya CD au DVD ya sauti, huenda DIGITAL AUDIO OUT (OPTICAL) isiweze kutoa mitambo ya sauti.