Huwezi kuunganisha kwa Intaneti, lakini sio kwa programu na huduma nyingine.
- Mipangilio ya tarehe na saa ya TV hii huenda isiwe sahihi. Kulingana na programu na huduma nyingine, huenda usiweze kuunganisha kwenye programu na huduma hizo ikiwa saa si sahihi.
- Hakikisha kwamba kebo ya LAN na waya ya nishati ya AC (waya kuu) ya kipanga njia/modemu* imeunganishwa vizuri.
- Kipanga njia/modemu yako lazima iwekwe ili iunganishe kwenye Intaneti. Wasiliana na mtoa huduma wako wa Intaneti kwa mipangilio ya kipanga njia/modemu.
- Jaribu kutumia programu baadaye. Seva ya mtoa maudhui ya programu huenda isiwe inafanya kazi.
Kidokezo
- Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya usaidizi ya Sony. Tovuti ya Msaada