Shughuli zimekatishwa, au kifaa hakifanyi kazi.
- Angalia ikiwa kifaa kimewashwa.
- Badilisha betri za kifaa.
- Sajili upya kifaa.
- Vifaa vya Bluetooth hutumia bendi ya 2.4 GHz, kwa hivyo kasi ya mawasiliano huenda ikapungua au kukatishwa mara kwa mara kwa sababu ya uhitilafianaji wa LAN pasiwaya.
- Huenda runinga au kifaa kisifanye kazi kwenye rafu ya chuma kwa sababu ya mwingiliano wa mawasiliano ya pasi waya.
- Kwa umbali unaoweza kutumika wa mawasiliano kati ya TV na vifaa vingine, rejelea mwongozo wa maagizo ya kifaa.
- Wakati vifaa kadhaa vya Bluetooth vimeunganishwa kwenye TV, ubora wa mawasiliano ya Bluetooth huenda ukapungua.