Chapisha

TV inakataa kuwaka.

Tekeleza taratibu katika mpangilio ulio hapa chini hadi utatue shida.

1. Angalia kama TV inawaka kwa kutumia rimoti.

Ekeleza rimoti kwenye sensa iliyo mbele ya TV na ubonyeze kitufe cha nishati kwenye rimoti.
Angalia kama TV itawaka au kama LED ya kuangaza itawaka.
Ikiwa LED ya kuangaza itawaka lakini TV ikose kuwaka, jaribu kuweka upya (kuwasha upya) TV.

2. Angalia kama TV inawaka kwa kutumia kitufe cha nishati kwenye TV.

Bonyeza kitufe cha nishati kwenye TV na uangalie kama TV itawaka. Kitufe cha nishati kiko kwenye upande au nyuma ya TV.
Kwa maelezo, rejelea Reference Guide ya TV.
Ikiwa TV itawaka kwa kutumia utaratibu huu, huenda kuna tatizo na rimoti. Rejelea mada hii.

3. Chomoa kebo ya umeme ya AC (kebo kuu).

Chomoa waya wa nishati ya TV (kebo kuu) kwenye soketi ya umeme. Kisha ubonyeze kitufe cha nishati kwenye TV na usubiri kwa dakika 2 na uchomeke waya wa nishati (kebo kuu) kwenye towe ya umeme.

Kidokezo

  • Wakati unachomoa TV na kuichoma tena kwenye umeme, huenda TV isiweze kuwaka kwa muda hata kama umebonyeza kitufe cha nishati kwenye rimoti au TV. Hii ni kwa sababu inachukua muda kuanzisha mfumo. Subiri kwa sekunde 10 hadi 20, kisha ujaribu tena.