Chapisha

Picha iliyoharibika./Skrini humemeka.

Kagua muunganisho na mkao wa antena (kinasa mawimbi) na vifaa vya ziada

  • Angalia muunganisho wa antena (kinasa mawimbi)/kebo.
  • Weka kebo ya antena (kinasa mawimbi)/mbali na kebo nyingine zinazounganisha.
  • Wakati unasakinisha kifaa cha hiari, wacha nafasi kati ya kifaa na TV.
  • Hakikisha kwamba antena (kinasa mawimbi) imeunganishwa kwa kutumia kebo ya coaxial ya 75-ohm ya ubora wa juu.

Kagua mpangilio wa [Mwendo]

  • Bonyeza kitufe cha ACTION MENU, kisha uchague [Picha] — [Mipangilio bora] — [Mwendo] — [Motionflow] — [Zima]. (Kwa modeli zinazokubaliwa na [Motionflow] pekee)
    Modeli zinazotangamana na [Motionflow] zina [Motionflow] katika [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Picha] — [Mipangilio bora] — [Mwendo].
  • Badilisha mpangilio wa sasa wa [Modi ya filamu] kuwa [Zima].
    Bonyeza kitufe cha ACTION MENU, kisha uchague [Picha] — [Mipangilio bora] — [Mwendo] — [Modi ya filamu].
  • Angalia mipangilio ya [Uwekaji kabla wa programu mwenyewe].
    Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Kutazama runinga] — [Idhaa] — [Usanidi wa Idhaa] — [Uwekaji wa analogi] — [Uwekaji kabla wa programu mwenyewe].
    • Weka [LNA] kwa [Zima] ili uboreshe mapokezi ya picha. (Huenda [LNA] isipatikane kulingana na hali/eneo/nchi yako.)
    • Tekeleza [AFT] ili kuboresha picha ya mapokezi ya analogi.
      (Upatikanaji wa [Uwekaji kabla wa programu mwenyewe] na chaguo zake unaweza kutofautiana kulingana na eneo/nchi/hali.)