Chapisha

Ukubwa wa skrini/Umbizo la skrini/Hali pana hubadilika kiotomatiki.

Unaweza kurekebisha ukubwa wa picha kutoka [Skrini].
Bonyeza kitufe cha HOME, kisha uteue [Mipangilio] — [Onyesho na Sauti] — [Skrini].

  • Wakati unabadilisha ingizo la kituo au video, ikiwa [Pana Oto] in [Skrini] imewezeshwa, mpangilio wa sasa wa [Modi Pana] hubadilishwa kiotomatiki kulingana na ishara ya ingizo. Ili ufunge mpangilio wa [Modi Pana], lemaza [Pana Oto].
  • Unaweza kurekebisha mwenyewe ukubwa wa picha kutoka [Modi Pana].

Mfano wa mpangilio [Modi Pana] (wakati mgao wa picha halisi ni 4:3)

  • [Kawaida]
    Huonyesha picha halisi kama ilivyo. Pau za kando ambazo hujaza utofauti katika picha ya 4:3 huonyeshwa upande wa kushoto na upande wa kulia mwa skrini.
    Example of setting
  • [Kuza]
    Huonyesha picha ya 16:9 ambayo imegeuzwa katika umbizo la kisanduku cha barua cha 4:3, katika mgao sahihi.
    Example of setting
  • [Kuza Pana]
    Hupanua picha, kwa kuhifadhi picha halisi kama iwezekanavyo.
    Example of setting

[Modi Pana] (wakati mgao wa picha halisi ni 16:9)

Huenda picha ikakosa kuonyeshwa kama ilivyokusudiwa hata kama ina mgao wa 16:9. Badilisha mipangilio ili kubadilisha kwa onyesho unalotaka.

  • [Kawaida]
    Huonyesha picha ya 4:3 ambayo ilipanuliwa wima katika 16:9, katika mgao sahihi.
    Example of setting
  • [Kuza]
    Huonyesha picha ya 16:9 ambayo imegeuzwa katika umbizo la kisanduku cha barua cha 4:3, katika mgao sahihi.
    Example of setting
  • [Kuza Pana]
    Hupanua picha, kwa kuhifadhi picha halisi kama iwezekanavyo.
    Example of setting

Kumbuka

  • [Pana Oto] katika [Skrini] hadi [Kuza Pana] auv[Kuza], ambayo itaendelea kutumika hadi ubadilishe kituo/ingizo au wewe mwenyewe ubadilishe tena mpangilio wa [Modi Pana].
  • [Pana Oto] katika [Skrini] haitapanua picha wakati wa kuswichi maudhui, kwa sababu maelezo ya maudhui yanadhibitiwa na mhudumu wa ishara ya idhaa. Unaweza kubadilisha kwa mkono mpangilio wa [Modi Pana] ikiwezekana, ambayo itasalia kwenye utekelezaji hadi ubadilishe idhaa/kiingizo au ubadilishe kwa mkono mpangilio wa [Modi Pana] tena.
  • Ukubwa wa picha hutegemea maudhui ya mawimbi.
    • Picha huwa ndogo zaidi wakati wa matangazo ya kibiashara kwa sababu ya mbinu iliyotumika namhudumu wa maudhui ya kutangaza. Wakati maudhui ya idhaa ya HD yanabadilika kuwa maudhui ya SD (matangazo ya kibiashara), picha inaweza kuwa ndogo na kingo nyeusi.
    • Baadhi ya vipindi vya skrini pana vinawekwa kwenye filamu kwa uwiano wa kipengele ambavyo ni vikubwa kuliko 16:9 (hii haswa ni kawaida na maonyesho ya miondoko). TV yako itaonyesha vipindi hivi na bendi nyeusi juu na chini ya skrini. Kwa maelezo zaidi, angalia nyaraka zilizokuja na BD/DVD yako (au wasiliana na mtoa huduma wako wa vipindi).
    • Vipindi vinavyotangazwa katika mifumo ya HD (720p na 1080i) na maudhui ya 4:3 kwa kawaida itakuwa na bendi nyeusi katika pande za kushoto na kulia kwenye skrini ambazo zinaongezwa na mtangazaji.

Kidokezo

Baadhi ya kebo na visanduku vya setileti vya kubadilisha analogi hadi dijitali vinaweza pia kudhibiti ukubwa wa picha. Kama unatumia kisanduku cha kubadilisha analogi hadi dijitali, rejelea mtengenezaji wa kisanduku cha kubadilisha analogi hadi dijitali kwa maelezo zaidi.