Chapisha

Kutumia Mwongozo wa Usaidizi

Mwongozo Huu wa Usaidizi unafafanua jinsi ya kutumia TV hii. Unaweza pia kurejelea Setup Guide kwa maelezo kuhusu kusakinisha TV, na Reference Guide kwa maelezo ya vipande, ainisho, na kuweka TV hii kwenye ukuta.

Katika Mwongozo huu wa Usaidizi, unaweza kusoma taarifa unayotaka au kuitafuta moja kwa moja. Ili utafute, teua the search icon juu ya skrini.

Matoleo ya Mwongozo wa Usaidizi

Kuna matoleo mawili ya Mwongozo wa Usaidizi wa TV yako: Mwongozo wa Usaidizi Ulioundiwa Ndani na Mwongozo wa Usaidizi wa Mtandaoni. Ili uangalie Mwongozo wa Usaidizi wa Mtandaoni, lazima TV yako iwe imeunganishwa kwenye Intaneti. Ili ubadilishe kati ya matoleo Yaliyoundiwa ndani na ya Mtandaoni, tumia kitufe cha kubadilisha (A) kilicho juu ya skrini. Unaweza kukagua ni Mwongozo upi wa Usaidizi unaoonyeshwa kwa sasa kwa kuangalia kichwa kilicho juu ya skrini.

Illustration of the location of switch button A
  1. Unganisha TV kwenye Intaneti.
  2. Teua (A) ili ubadilishe toleo la Mwongozo wa Usaidizi.

Kumbuka

  • Ili utumie vipengele vipya vilivyofafanuliwa katika Mwongozo wa Usaidizi, huenda ukahitaji kusasisha programu ya TV. Kwa maelezo kuhusu visasisho vya programu, angalia ukurasa wa Sasisho za programu.
  • Majina ya mipangilio katika Mwongozo wa Msaada yanaweza kutofautiana na yale yanayoonyeshwa kwenye TV kulingana na tarehe ya toleo la TV au modeli/nchi/eneo lako.
  • Picha na vielelezo vinavyotumiwa katika Mwongozo wa Usaidizi huenda vikawa tofauti kulingana na modeli ya TV yako.
  • Muundo na ainisho zinaweza kubadilika bila notisi.

Kidokezo

  • Ili kuona kama TV yako ina moja ya vitendaji vilivyoelezewa katika Mwongozo wa Usaidizi, rejelea mwongozo wa karatasi au katalogi ya bidhaa ya Sony.
  • Mwongozo huu wa Usaidizi umeandikiwa maeneo/nchi zote. Baadhi ya maelezo yaliyo katika Mwongozo huu wa Usaidizi hayatumiki kwa maeneo na nchi nyingine.