Chapisha

Kufahamu misingi ya TV ya 3D (modeli za 3D tu)

Modeli za 3D zina [Mipangilio ya 3D] katika [Mipangilio] — [Onyesha].

Umbali unaopendekezwa wa kutazama wa taswira ya 3D

Ikiwa umbali wa kutazama haufai, huenda taswira mbili zikatokea. Keti angalau umbali wa mara 3 urefu wa skrini mbali na TV. Kwa utazamaji bora zaidi, tunapendekeza kwamba uketi moja kwa moja mbele ya TV.

Illustration of the best distance to watch TV

Kidokezo

  • Kuna aina mbili za Miwani ya 3D: Tulivu na Amilifu. Rejelea ainisho katika Reference Guide ili uone ni aina gani za miwani ya 3D ambayo TV inakubali.

Masafa ya mawasiliano ya runinga na Miwani Inayotumika ya 3D

Miwani inayotumika ya 3D huwasiliana na TV ili kukuonyesha picha katika 3D.

Mkao wako wa kutazama unahitaji kuwekwa katika masafa yanayofaa. Angalia picha zinazofuata. Umbali wa kufanya kazi unategemea vizuizi (watu, chuma, kuta, n.k.) na/au mwingiliano wa sumaku ya umeme.

  • Mwonekano wa juu
    Illustration of the communication range from an overhead view
    1. 120°
    2. 1-6 m (3-20 ft.)
  • Mwonekano wa upande
    Illustration of the communication range from a side view
    1. 45°
    2. 1-6 m (3-20 ft.)
    3. 30°

Kumbuka

  • Mtazamo wa kuona na umbali unaopendekezwa huenda ukatofautiana kulingana na eneo la runinga na hali za chumba.

Kutunza miwani yako

  • Pangusa miwani kwa umakini na kitambaa laini.
  • Madoa sugu yanaweza kuondolewa kwa kitambaa chenye unyevu wa sabuni kidogo na maji ya vuguvugu.
  • Ikiwa unatumia kitambaa kilichotibiwa kwa dawa, hakikisha unafuata maagizo yaliyo kwenye pakiti.
  • Usitumie kamwe miyeyusho kama vile thina, kileo a benzene kwa usafishaji.