Chapisha

Kurekodi kwa kipima saa (modeli za kurekodi za USD HDD tu)

Modeli za kurekodi USB HDD zina [Usanidi wa kifaa cha kurekodi] katika [Mipangilio].

Kumbuka

  • Kitendaji hiki kinapatikana tu kwenye baadhi ya modeli barani Ulaya, Australia na nchini Nyuzilandi.
  1. Bonyeza kitufe cha GUIDE.
  2. Chagua kipindi unachokipenda katika mwongozo wa kipindi, kisha uteue [REK ya Kipimaji Muda].
  3. Chagua [Weka Kipima Saa Kama Tukio] au [Weka Kipanga Saa].

Ili kuweka wewe mwenyewe kipima saa kwa kubainisha tarehe, saa na kituo

  1. Bonyeza kitufe cha GUIDE.
  2. Sogeza uangazishaji hadi kushoto kwa kipengee, kisha usonge kushoto hadi ufungue menyu.
  3. Chagua [Orodha ya Kipima Saa] — [REC kwa Kipimasaa].
  4. Sanidi mpangilio wa kipima saa.
  5. Teua [Weka Kipanga Saa].

Ili ukague, urekebishe au ufute mipangilio ya kipima saa

Kuangalia, kurekebisha, au kufuta mipangilio ya kipima saa hutekelezwa katika [Orodha ya Kipima Saa].

  1. Bonyeza kitufe cha GUIDE.
  2. Sogeza uangazishaji hadi kushoto kwa kipengee, kisha usonge kushoto hadi ufungue menyu.
  3. Chagua [Orodha ya Kipima Saa], kisha ubadilishe mipangilio.

Kidokezo

  • Hadi mipangilio 32 ya kipima saa inaweza kuundwa.
  • Rekodi ikishindikana, sababu itaorodheshwa katika [Orodha ya Hitilafu za Kurekodi]. Bonyeza kitufe cha TITLE LIST, kisha uchague [Orodha ya Hitilafu za Kurekodi].
  • Katika mwongozo wa vipindi, unaweza kusogeza lengo hadi kwenye kipindi unachokitaka na ubonyeze kitufe cha REC ili uweke kipima saa cha rekodi cha kipindi.

Kumbuka

  • Kipima saa cha rekodi hakitafanya kazi wakati kebo ya AC (waya kuu) imechomolewa.