Chapisha

Kutoa sauti kutoka mfumo wa sauti

Unaweza kuunganisha mfumo wa sauti kama vile vipokea AV au miambaa ya sauti kwenye TV. Chagua mbinu ya muunganisho hapa chini kulingana na ainisho za mfumo wa sauti unayotaka kuunganisha.

  • Kuunganisha kwa kutumia kebo ya HDMI (Kwa maelezo, soma kwa makini “Muunganisho kwa kutumia kebo ya HDMI” hapa chini.)
  • Kuunganisha kwa kebo optiki ya dijitali
  • Kuunganisha kwa kebo ya sauti

Kwa mbinu za muunganisho, rejelea ukurasa wa Kuunganisha mfumo wa sauti.

Kumbuka

  • Rejelea mwongozo wa maagizo ya kifaa cha kuunganishwa.

Muunganisho kwa kutumia kebo ya HDMI

Kifaa hiki kinakubali Audio Return Channel (ARC). Unaweza kutumia kebo ya HDMI ili kutoa sauti kutoka kwenye mifumo ya sauti ambayo inakubali ARC.

Kwa mbinu za muunganisho, rejelea ukurasa wa Kuunganisha mfumo wa sauti.

Kumbuka

  • Eneo la temino ya HDMI ambayo inakubali ARC hutofautiana kulingana na modeli. Rejelea mwongozo uliojumuishwa wa marejeleo.