Chapisha

Kurekebisha mipangilio ya BRAVIA Sync

  1. Washa kifaa kilichounganishwa.
  2. Kuwezesha [Udhibiti wa BRAVIA Sync], bpnyeza kitufe cha HOME, kisha uchague [Mipangilio] — [Ingizo za nje] — [Mipangilio ya BRAVIA Sync] — [Udhibiti wa BRAVIA Sync].
  3. Wezesha BRAVIA Sync kwenye kifaa kilichounganishwa.
    Wakati kifaa maalum kinachotangamana na Sony BRAVIA Synckimeunganisha na kuwashwa na [Udhibiti wa BRAVIA Sync] imewezeshwa, BRAVIA Sync huwezeshwa kiotomati kwenye kifaa hicho. Kwa maelezo, rejelea mwongozo wa maagizo wa kifaa kilichounganishwa.

Chaguo zinazopatikana

Chaguo zinazopatikana huonyeshwa hapa chini. (Chaguo hutofautiana kulingana na modeli/eneo/nchi yako.)

[Uzimaji oto wa vifaa]
Ikilemazwa, kifaa kilichounganishwa hakizimwi kiotomatiki wakati TV imezimwa.
[Uwashaji oto wa Runinga]
Ikilemazwa, TV haiwaki kiotomatiki wakati kifaa kilichounganishwa kimewashwa.
[Badiliko la ingizo oto (MHL)] (modeli zinazokubaliMHL pekee)
Ikiwezeshwa, ingizo ya TV hubadilisha moja kwa moja kwenye kifaa kingine kilichounganishwa kwa kutumia kebo ya MHL.
[Orodha ya kifaa cha BRAVIA Sync]
Huonyesha orodha ya vifaa vya BRAVIA Sync.
[Funguo za kudhibiti kifaa]
Hukuruhusu uweke vitufe vya kudhibiti kifaa kilichounganishwa cha HDMI au MHL (modeli zinazokubali MHL pekee).
[Kuchaji kwa MHL wakati wa kusubiri] (modeli zinazokubaliMHL pekee)
Ikiwezeshwa, TV inaweza kuchaji kifaa kilichounganishwa cha MHL wakati tv iko katika hali ya kusubiri.

Ili utumie Menyu landanifu

  1. Bonyeza kitufe cha ACTION MENU, chagua Menyu landanifu, na uteue kipengee unachotaka katika Menyu landanifu.

Kidokezo

  • Katika masuala yafuatayo, ujumbe hutokea kwenye skrini ya TV unapochagua Menyu landanifu.
    • Kifaa cha HDMI au MHL (modeli zinazokubali MHL pekee) haijaunganishwa.
    • [Udhibiti wa BRAVIA Sync] imelemazwa.